نهاية التدليس في مقتل الخليفة ذي النورين
الجزء ١ · صفحة ١١٦anajua kuwa hii ni KAULI MAARUFU katika madhehebu ya Imaam MAALIK!! Bali ni kauli maarufu ya SAHABA ABDULLAH BIN ZUBEIR kama ilivyotajwa katika kitabu cha BIDAAYATUL-MUJTAHID cha IBNI-RUSHD!!!
Halafu tena wakajitokeza akina-SALIM BARHAYAAN، KASSIM MAFUTA، MOHAMED MAFUTA wote hao ni mawahabi wa Tanga-Tanzania، akaja mwengine ABDALLA BIN HUMEID wa KENYA naye alikuja akawazulia IBADHI kuwa wanaitikadi ya kutumia maji mengi katika josho la janaba!!! Yaani: Hujui ucheke au ulie!! UONGO MZANDIQ!! Na mtu hana haya usoni mwake hata chembe!!!
Ikisha akaja mwengine anaitwa NZIGAMASABO HUSSEIN wa BURUNDI (huyu si wahabi) naye akaboronga katika suala la MASAHABA na mengineyo، na hivi karibuni katokea ABDUL-QAADIR AL-AHDAL wa Daresalaam naye akajivuika katika pote la TAKFRIYYIIN!!! Wote hao tuliwatandika baada ya kupotosha HAQQI.
Kabla ya kufikia tamati niseme tu: SUALA LA MASAHABA USALAMA NI KUNYAMAZA!! WENZETU WANAOJARIBU KULIHUSISHA NA SISI AHLIL-HAQQ (IBADHI) TU TUTAWAFUMUA VIBAYA SANA KWA HOJA ZENYE NGUVU KAMA ULIVYOONA KATIKA KITABU HICHI KWA USHAHIDI KAMILI na pia litawabakisha siku zote WAWE WAONGO KWA KUKATAA UKWELI WANAOUJUA.
Mwisho، nimbashirie Msomaji wetu mpenzi kuwa tayari nimekaribia kumaliza kuhariri kitabu kinachohusiana na msimamo wa MAULAMAA kwa masahaba kwa jumla na MUAAWIYA hususan، na kitabu chengine cha tarekhe (historia) kwa mukhtasari. Allah atupe uhai na nguvu tuweze kuvichapisha ili haki iweze kueleweka.
26 RAJAB 1445 sawa na 7 FEB 2024
116