نهاية التدليس في مقتل الخليفة ذي النورين
الجزء ١ · صفحة ١١٥AHLUL-HAQQ (MAIBADHI) akawasihi watu waende Oman wakaone namna OTHMAAN anavyosemwa!!!
Maskini nyii!! Ni mvurumishaji tu hajui hata anachokizungumzia!!! Hajui siasa wala sera za nchi ya Oman wala MADHEHEBU YA KIIBADHI katika masuala kama haya!! Haelewi kuwa watunzi wa vitabu wanavyovisomesha misikitini mwao vinawatwanga baadhi ya masahaba kisawa-sawa!! Nitoe mfano mmoja tu hapa، ASSAN-'AANIYY mtunzi wa kitabu mashhuri cha SUBULI SSALAAM katika diwani la mashairi yake katangaza kwa kula KIAPO KUWA MUAAWIYA ni FAASIQ، SHETANI MKOROFI، na MLAANIFU!!!
Lakini siajabu kwa kijana huyu MOHAMMED BACHUU، kwani pia alidai kuwa IBADHI na wengine wanawakafirisha waislamu kwa suala la kuacha sala!! Kumbe hiyo ndio kauli na madhehebu ya shekhe wake mpendwa UTHAIMEEN!!! Ujinga wake ni huo halafu eti yeye ndio mmoja wa mawakala wa kueneza UWAHABI Zanzibar!!!
BACHUU huyu huyu aliwahi kumtia makosani SH. NASSOR BACHUU kwa kuwa na ITIKADI YA KUTOTOKA MOTONI KWA MUISLAMU ANAYEKUFA NA MADHAMBI MAKUBWA BILA YA KUTUBIA، halafu akamtakia rehma na maghfira!!
Ilhali anajua fika kuwa katika UWAHABI itikadi hii ni UPOTOFU USIOSAMEHEKA!! Wala haumbakishi mtu kuwa tena katika AHLI- SUNNA au SALAFIA!!! Jee zile REHMA alozomtakia ni kwa ajili ni BABA YAKE??? Lakini wengine anawaumbua kwa madogo kuliko hayo!!!
MOHAMMED BACHUU ni mdogo sana، wako waliomtangulia، alianza Mzee wake SH. NASSOR BACHU akasema kuwa wale wenye kusali wakiachia mikono ni kama MINAZI NA MIPOPOO!!! Kweli haya ni maneno ya kielimu hayo?? Ilhali mwenye uono mdogo tu wa fiqhi
115