ذكرى محمد صلى الله عليه وسلم سلطان بن مبارك بن حمد الشيباني

10. ذكرى محمد صلى الله عليه وسلم (باللغتين العربية والسواحلية)

الجزء ١ · صفحة ٣٣

32

1

Alisifika Mtume tangu utotoni mwake kwa ukweli na uaminifu na kutofanya baya lo lote hata akatangaa kwa jina la Al-Amin. Na alikuwa mnyenyekevu hana kibri، hamdharau mtu. Hata masikini anakwenda kuwatazama wanapokuwa wagonjwa na anakaa nao mahala Pamoja. Na anachanganyika na Masahaba wenzake kama mwenzao. Anakaa po pote pale anapofikia. Si lazima akae Sadrul Majlis. Alikuwa karimu kuliko viumbe wote، mpole kuliko viumbe wote، msema kweli kuliko viumbe wote، mwepesi wa tabia kuliko viumbe wote، mtekelezaji ahadi kuliko viumbe wote. Ukimwona kwa ghafla utamwogopa، ukizoeleana naye utampenda.

Moja katika ya kuonyesha ukarimu wake ni kuwa siku moja aliweka mbele yake juu ya mkeka dirham 90،000 (tisiin alfu) akazigawa zote pale pale.

kama alivyosema

Alikuwa mpole kabisa Mwenyezi Mungu na akawa na tabia zisizokuwa na mfano wake vile vile kama alivyosema Mwenyewe Mwenyezi Mungu. Basi yeye Nabii Muhammad ndiye bora kuliko viumbe wote.