ذكرى محمد صلى الله عليه وسلم سلطان بن مبارك بن حمد الشيباني

10. ذكرى محمد صلى الله عليه وسلم (باللغتين العربية والسواحلية)

الجزء ١ · صفحة ٣٤

33

Na

alistahamili adha kubwa kabisa kwa

Makureshi katika kuitangaza dini. Walimtaka kila namna ajizuilie na hayo; asikubali. Wakahadid kuwa watamwua baada ya kumtaabisha hivyo walivyokuwa wakimtaabisha. Hata Ami yake، Bwana Abu Talib، alipomnasihi ayaache hayo alimwambia "Hata lau wangenitilia jua kwenye mkono wangu wa kulia na mwezi katika mkono wangu wa kushoto ili niache haya nisingeacha mpaka nife".

Alipotimiza umri wa miaka 38 alijiepusha kukaa na watu. Akawa anakaa kwenye pango lililokuwa likiitwa Ghar Hira akiabudu humo. Na hivi ndivyo wanavyokuwa watu wakubwa wa Mwenyezi Mungu. Wakawa tayari kupokea ule ujumbe wa Mwenyezi Mungu wa kuwatoa watu ukafirini na ujingani na matatani. Hata alipotimiza miaka 40 alipewa Utume juu ya viumbe wote uwaonye waovu awabashiri wema، awatoe katika ujahili awatie katika ujuzi. Na haya yalikuwa katika mwezi wa February mwaka 610 A.D.

Na muujiza mkubwa kabisa kabisa aliopewa Mtume ni huu muujiza wa Quran. Kitabu kitukufu cha