ذكرى محمد صلى الله عليه وسلم سلطان بن مبارك بن حمد الشيباني

10. ذكرى محمد صلى الله عليه وسلم (باللغتين العربية والسواحلية)

الجزء ١ · صفحة ٣٥

34

Mwenyezi

Mungu kilichowashangaza viumbe

vyote visifue dafu mbele yake juu ya ufasihi wao na uhodari wao na ubingwa wao.

Akaingia Mtume kuwalingania watu dini kwa hikma na upole na mawaidha mazuri na kusubiri juu ya kila balaa na maafa yaliyokuwa yakimpata yeye na hao wafuasi wake. Basi ni uzushi na uwongo mkubwa kabisa kusema kuwa dini ya Kiislamu imetangaa kwa upanga. Upanga gani huo alioukamata Mtume kuchinja watu ili waingie Uislamuni? Mtume alikuwa hawezi kujinusuru mwenyewe wala kuwanusuru hao wafuasi wake. Ataweza kuwapiga watu wengine? Hakukimbia yeye Mtume peke yake na Sayyidna Abubakr kwenda Madina kwa ajili ya kukimbia kuuawa na Makureshi? Basi upanga huo au panga hizo zilikuwako wapi?

Muda wa miaka 13 kasimama Mtume kulingania watu dini، hana silaha yoyote ila Imani yake tu juu ya Mwenyezi Mungu. Na ikamkuta kila balaa yeye na watu wake; hata wengine wakauawa na wengine wakarejea ukafirini balaa zilipopindukia mipaka. Hawakusalia pamoja naye ila wale ambao nyoyo zao