ذكرى محمد صلى الله عليه وسلم سلطان بن مبارك بن حمد الشيباني

10. ذكرى محمد صلى الله عليه وسلم (باللغتين العربية والسواحلية)

الجزء ١ · صفحة ٣٦

35

zilijaa Uislamu kweli kweli na kumtawakali Mwenyezi

Mungu.

Basi watu hao walimfuata Mtume kwa ajili ya upa nga? Alikuwa na upanga yeye Mtume? Au upanga tangu lini unathibitisha itikadi katika nyoyo? Au watu hawa walisilimu kwa tamaa ya pesa? Mtume alikuwa na pesa kwani hata wamfuata kwa tamaa ya pesa?

Wote hawa walisilimu kwa kuwa wameathirika

kwa ile taalimu

nzuri kabisa ya

sio wameathirika kwa jambo jengine.

66

Uislamu

Walidumu Waislamu juu ya fitna hiyo na dhulma hiyo waliyokuwa wakifanyiwa na makafiri - na kila siku inazidi tu. Hata ilipopindukia mipaka ndipo Mwenyezi Mungu akawapa ruhusa Waislamu wajitetee nafsi zao na waihami dini yao. Akasema Wamepewa ruhusa wale waliokuwa wanapigwa (wajipiganie na wao) kwani wanadhulumiwa bure na Mwenyezi Mungu ni Qadir wa kuwanusuru; ambao wametolewa katika miji yao pasina haki yo yote. Ila walisema “ Mola wetu ni Mwenyezi Mungu (si masanamu)”. Na akasema “Piganeni nao (kama wanavyokupigeni) hata