نهاية التدليس في مقتل الخليفة ذي النورين
الجزء ١ · صفحة ١١٠MUKHTASAR WA KITABU
Kitabu hichi (MWISHO WA UBABAISHAJI KATIKA MAUWAJI YA KHALIFA DHUU-NNUURAIN) kinazungumzia tokeo kubwa lililotokea katika historia ya kiislamu mwaka 35 H، nalo ni tokeo la kuuwawa kwa KHALIFA WA TATU: OTHMAAN BIN AFFAAN.
Namshukuru ALLAH kuwa pasi na kutarajia kitabu hichi kimefika OMAN، ALGERIA، LIBYA na hata kusomeshwa nchini GHANA، si hivyo tu bali kubadilisha watu mielekeo yao juu ya suala hili.
Wengi wanapolizungumzia tokeo hili huleta taswira ya kuondoshana njiani kuwa KHALIFA huyo kauliwa na watu wasiotambulikana، watu wasio na dini، watu washenzi، na makapikapi ya makabila!! Na kuwa hakuna sahaba hata mmoja aloshiriki katika mauwaji ya SAHABA OTHMAAN!!
Waswahili husema: "NJIA YA MUONGO NI FUPI” kupitia kijitabu hichi kidogo tunakuta MAULAMAA KEM-KEM WA AHLI-SUNNA WAL-JAMAA wamebainisha majina kadhaa ya masahaba wakubwa walioshiriki katika KUMZINGIRA KHALIFA WA TATU nyumbani kwake mpaka kuuliwa kwake!!!
Ndugu Msomaji! Huwezi kuamini kabisa kuwa WALIOMZINGIRA NA KUMUUWA KHALIFA OTHMAAN ni mseto baina ya MASAHABA WAKUBWA NA MATAABIINA WEMA KABISA!!!
Unaweza kusema umepata wapi IBADHI wewe UZUSHI huu!!! Mbona mmezidi!!!
Wallaah، Billaahi، Taallaahi!! Hatukuzidi wala kupungua huo ndio ukweli uliokuwepo katika vitabu vilivyohaririwa na MAULAMAA WA KIISLAMU wakiwemo wa AHLU-SUNNA!! Sasa tutafanya nini?? NA UKWELI SIKU ZOTE UNAUMA!! Hebu mwangalie IBNU-KATHEER anavyosema katika kitabu chake maarufu cha AL-BIDAAYA WANNIHAAYA (7/172 - 173)، anasema:
WALIKUWA WAKIMTUKANA OTHMAAN NA SAID BIN AL-AAS، NA WALIKUWA KUMI، na imesemwa kuwa walikuwa TISA، na hii ndio kauli iliyofanana (kuwa sahihi)، miongoni mwao ni:
110