نهاية التدليس في مقتل الخليفة ذي النورين خلفان بن سليمان بن خلفان الطيواني أبو الطيب

نهاية التدليس في مقتل الخليفة ذي النورين

الجزء ١ · صفحة ١١٢

1 - KUMAIL BIN ZIYAAD

2 - ASHTAR ANNAKHAI (MAALIK BIN YAZEED).

3 - ALQAMA BIN QAYS ANNAKHAI

4 - JUN-DUB BIN KA'AB AL-AAMIRIYY

5 - 'URWA BIN AL-JA'AD

6 - 'AMRY BIN AL-HAMIQ

7 - SA'ASA-'A BIN SUUHAAN

8 - NA NDUGU YAKE: ZAYD BIN SUUHAAN

9 - IBNU-KAWWAA

WAKAFIKILIA AL-JAZIIRA، KISHA WAKAHAMIA HIMS MPAKA IKAJA FITNA WALIYOIONGOZA YA KUMUUA OTHMAAN".

Mwisho wa kunukuu!! MSOMAJI WA KAWAIDA hadi kufikia hapa hawezi kuona ndani!!! Mpaka apate mtu wa kumfunua macho، na kumzibua masikio!! Na mimi ndio kazi niliyokuja nayo hiyo، ya kufunua watu macho na kuzibua mashikio!! Na kuwasafisha tongo kwa brush laini isiyoumiza ili waijue HAKI na waache KASUMBA، MBWE-MBWE BANDIA pale wanapokuwa juu ya MEMBAR au KUDARISISHA KUHUSU FITNA ZILIZOTOKEA KIPINDI CHA MASAHABA!!!

Narejea tena kusema kuwa MSOMAJI wa KAWAIDA hapo haambulii (hapati) kitu، hapo mpaka tumhijishe (ALIF، BEE، TEE) kwani anaendelea kusikia MATUSI، SHUTMA na HUJUMA mbali-mbali dhidi ya wale WATU TISA au KUMI!!

Na anafahamishwa kuwa hao ndio VINARA WA VITNA ZA KUMUUWA KHALIFA WA TATU OTHMAAN BIN AFFAAN.

Sasa NDUGU MSOMAJI kaa mkao wa kusoma، na kuhifadhi uambiwayo، nikuambie kuwa hao watu KUMI (10) au (9) miongoni mwao ni:

1 - MASAHABA (WALIOANDIKWA KWA RANGI YA BULUU).

2 - MATABIINA WEMA.

112