نهاية التدليس في مقتل الخليفة ذي النورين خلفان بن سليمان بن خلفان الطيواني أبو الطيب

نهاية التدليس في مقتل الخليفة ذي النورين

الجزء ١ · صفحة ١١٣

•

•

NA WAO NDIO WALIONGOZA KATIKA KUMZINGIRA OTHMAN MPAKA KUULIWA KWAKE.

NA WAO NDIO WALIOMSIMAMISHA ALIYY KWENYE UKHALIFA.

• NA NDIO WATU WA ALIYY WA KARIBU KATIKA UKHALIFA WAKE، NA WENGINE NDIO MAJEMEDARI JESHI WAKE!!!

Jee huoni Ndugu Msomaji kuwa hichi pekee ni na kitandawili cha tega- tegua!!

Yaani ALIYY BIN ABII TAALIB katika kipindi chake chote cha miaka mitano mpaka kuuliwa kwake hajanyanyua mkono wake dhidi ya waliohusika na MAUWAJI YA OTHMAAN، bali watuhumiwa hao ndio wandani wake katika vita na amani!!!

Hii inamaanisha nini??? Ni dhahiri kuwa ALIYY K.W hakuona kuwa kuna mtuhumiwa anayestahiki kusimamishiwa KISASI kwa mauwaji waliyoyafanya، na ndio maana alikubali kuingia katika vita vikubwa vya waasi wa SHAAM vilivyoongozwa na MUAAWIYA!!! Na hakuwa tayari kutoa mtuhumiwa hata mmoja!!!

Lakini kijitabu hichi pia kimegusia suala nyeti la kuwasema MASAHABA، ambalo MAPOTE mengine wameliingiza kwenye vitabu vya AQIDA!!! Na kudai kuwa ni RED LINE hawafai katu kuguswa!!!

Lakini ukiingia ndani ya vitabu vya SIRA، TARJAMA، HISTORIA na TAFSIRI utakuta mkururo wa MAULAMAA WA AHLI-SUNNA waliokuwa wakiwasema، na kuwatukana masahaba kinaga-ubaga tena katika utafauti wa madhehebu na itikadi zao!!!

Nakusudia kusema MAHANAF، MAALIK، MASHAFI، MAHANBAL، lakini pia tukija kwa mpangilio mwengine MAFAQIIHI، WATU WA HADITHI، MASUFI، MAWAHABI، ASHAAIRA، MAATURIDIYYA na wengineo hali ni hiyo-hiyo!!!

113